Waziri Kabudi akutana na Balozi Al - Mashaan

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Kuwait anayeshughulikia masuala ya Afrika, Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan.

Pamoja na mambo mengine walizungumzia kuhusu jinsi ya kuboresha mahusiano yaliyopo katika kati ya Tanzania na Kuwait, nchi ya Kuwait imekuwa ni kati ya wadau muhimu wa Maendeleo hapa nchini kupitia mradi wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait(Kuwait Fund). 


Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam tarehe 18 Juni, 2019

  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimwelezea jambo Balozi Hamad Suliman Al - MashaanWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimwelezea jambo Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan
  • Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi,Zanzibar pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wakifuatilia Mkutano wa 9 wa Jumuiya hiyo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Dar es Salaam,Tanzania. Kutoka kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa akifuatiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Aman Abeid Karume,akifuatiwa na Makamu wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu Dkt Mohamed Gharib Bilali,akifuatiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo.
  • Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan, Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohamed AlSehaijan (wa pili kutoka kulia) pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwaiti na Afisa Mambo ya Nje Bw. Odilo Fidelis (wa pili kutoka kushoto)Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) na Balozi Hamad Suliman Al - Mashaan, Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Mubarak Mohamed AlSehaijan (wa pili kutoka kulia) pamoja na maafisa Ubalozi wa Kuwaiti na Afisa Mambo ya Nje Bw. Odilo Fidelis (wa pili kutoka kushoto)