Resources » News and Events

Wananchi waendelea kujitokeza katika banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba

Mama Anna Mkapa Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa, akiangalia moja ya machapisho yanayopatikana katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya biashara ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Wananchi wengi wameendelea kujitokeza kwenye banda la Wizara ili kuongeza uelewa juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara, ikiwemo namna Wizara inavyosimamia na kuteleza sera ya mambo ya nje ya nchi, faida na hatua mbalimbali za mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lipo katika jengo la sabasaba hall.Wananchi wote wanakaribishwa

Wananchi waendelea kujitokeza katika banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba

  • Sehemu nyingine ya wananchi wakipata maelekelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara
  • Sehemu nyingine ya Wananchi wakipewa maelekelezo na mtumishi wa Wizara