Resources » Press Release

Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya umeandaa Misa Maalum ya kumbukumbu ya Mwalimu J.K Nyerere

TAARIFA KWA UMMA
Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya umeandaa Misa Maalum ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere itakayofanyika tarehe 14 Oktoba, 2017 katika Kanisa la Holy Family Basilica, Nairobi kuanzia saa 4.00 hadi saa 5.00 asubuhi.
Watanzania wote pamoja na ndugu, jamaa na marafiki mnakaribishwa kushiriki katika Misa hii. Kufika kwenu kwa wingi ndio kufanikisha shughuli yetu sote.
TUNATANGULIZA SHUKRANI ZETU ZA  DHATI.
IMETOLEWA NA:
UBALOZI WA TANZANIA
NAIROBI, KENYA
10 OKTOBA, 2017