Resources » News and Events

Tanzania ya tia fora kwenye Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki jijini Bujumbura

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania (waliovalia jezi nyeupe) ikichuana na timu ya wanawake ya mpira wa miguu ya Burundi katika uwanja wa mpira wa Gitega, Burundi. Katika pambano hili timu ya Taifa ya Tanzania iliibuka na ushindi mnono wa magoli 8-1 dhidi ya timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Burundi. Kufuatia ushindi huu timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania inatarajia kukutana na Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Kenya katika mchezo utakaofanyika siku ya Alhamis terehe 23 Agosti 2018 kwenye uwanja wa mpira wa Gitega, Burundi. Aidha, timu ya mpira wa pete ya Taifa ya Tanzania pia iliibuka na ushindi mnono wa magoli 79-14 dhidi ya timu ya mpira wa pete ya Burundi. Kufuatia shindi huo timu ya Taifa ya mpira wa pete inatarajia kukutana na timu ya mpira wa pete ya Uganda hapo kesho tarehe 22 Agosti, 2018 katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha ENS jijini Bujumbura Vilevile timu ya mchezo wa Karate ya Taifa nayo imeanza kushiriki mchezo huo katika hatua mbalimbali, ambapo hadi sasa mwenyeji wa tamasha hilo Burundi ndiye anayeongoza kushida kwenye vipengele vingi vya mchezo huo. Tanzania katika Tamasha hili inashiriki katika michezo minne tofauti ambayo ni Riadha (mashindano bado hayajaanza), mpira wa miguu (kwa timu ya wanawake pekee), karate na mpira wa pete. Tamasha la kwanza la Michezo la Afrika Mashariki lilianza kufanyika tarehe 15 Agosti na litafikia tamati Agosti 30, 2018 nchini Burundi.

Tanzania ya tia fora kwenye Tamasha la Michezo la Afrika Mashariki jijini Bujumbura

  • Timu ya mpira wa miguu ya Wanawake ya Tanzania ikishangilia ushindi pamoja mashabiki waliojitokeza kushuhudia shindano hilo
  • Timu ya mpira wa pete ya Tanzania (waliovalia jezi rangi ya bluu) ikiishambulia timu ya timu ya Burundi kwenye moja ya mchezo katika Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki. Katika pambano hilo Tanzania iliibuka na ushindi wa magoli 79 -14 dhidi ya Burundi