Resources » News and Events

Tamasha la kwanza la Michezo la Afrika Mashariki lazinduliwa jijini Bujumbura, Burundi.

Wanamichezo kutoka Tanzania wakipita kwa furaha mbele ya jukwaa kuu kwenye hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Kwanza la Michezo la Afrika Mashariki Tamasha hili linalofanyika kwa mara ya kwanza nchi Burundi limetokana na maagizo ya Mkutano wa 35 wa Baraza la Mawaziri la Afrika Mashariki. Tamasha hili lenye kauli mbiu "kujenga Jumuiya ya Afrika Mashariki na amani kupitia michezo" linafanyika kuanzia terehe 16 hadi 30 Agosti, 2018. Washiriki zaidi 1000 kutoka nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki watashiriki kwenye michezo mbalimbali ya tamasha hili. Tanzania imewakilishwa na jumla ya wanamichezo 58 ambao watashiriki katika michezo ya mpira wa pete, mpira wa miguu, riadha na karatee. Tamasha hili limefunguliwa tarehe 16 Agosti 2018 na Mhe. Dkt. Joseph Butore Makamu wa Pili wa Rais wa Jamhuri ya Burundi, katika viwanja vya Sekondari vya SOS jijini Burundi na kuhudhuriwa na viongozi na watendaji waserikali kutoka nchi wanachama.

Tamasha la kwanza la Michezo la Afrika Mashariki lazinduliwa jijini Bujumbura, Burundi.