Spika wa Bunge la Morocco atembelea Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt Augustine Mahiga akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Habib El Malki, anayefuatilia mazungumzo hayo ni Balozi wa Morocco nchini Mhe. Mhe. Abdelilah Benryane katika ukumbi wa VIP wa Uwanja wa ndege Dodoma, tarehe 9/12/2017. Katika mazungumzo yao Mhe. El Malki na Mhe. Waziri walizungumzia masuala mbalimbali ya kudumisha na kukuza ushirikiano wa kidiplomasia,uchumi na utalii.

Spika wa Bunge la Morocco atembelea Tanzania

  • Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Job Ndugai akimkaribisha Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Habib El Malki nyumbani kwake Mjini Dodoma, tarehe 9/12/2017
  • Mhe.Habib El Malki (wa kwanza kulia)-Spika wa Bunge la Morocco, Mhe. Job Ndugai- Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Zubeir Ali Maulid - Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Dkt. Suzan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pamoja na wajumbe wengine kutoka Ofisi ya Bunge na Ujumbe wa Morocco ulioambatana na Spika wa Morocco wakiwa katika mazungumzo Bungeni Dodoma, tarehe 9/12/2017. Katika mazungumzo hayo Mhe.El Malk alitoa mwaliko kwa Mhe. Ndugai na Mhe. Ali Maulid, Mhe. El Malki alisema amefurahishwa sana na jinsi alivyopokelewa na kwa umaalum zaidi alimshukuru Mhe. Rais kwa kumpa heshima ya kipekee kwa kumtambulisha kwa Umma wa Watanzania wakati wa sherehe za maadhimisho ya Uhuru. Mhe. El Malki alisema Morocco ina mengi ya kujifunza kwa Tanzania hasa katika eneo la Demokrasia "nimeshangazwa sana kuona Marais Waastafu wanakaa pamoja na kuunga mkono Rais aliye madarakani, hili ni jambo tunalopaswa kuiga hasa kwa nchi za Afrika, tumezoea kuiga mambo mengi kutoka nchi za Magharibi na kudharau mambo mazuri ambayo yako kati yetu" alisema Mhe. El Malki.