Regional Oversight Mechanism of the Peace, Security and Cooperation framework

Mheshimiwa Charles Mwijage (Mb.), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Mhe. Dkt. Damas NDumbaro (Mb.) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsalimia Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda huko Kampala tarehe 8 Oktoba, 2018 mara baada ya kukamilika kwa Mkutano wa Ngazi ya Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Maziwa Makuu katika mpango wa amani na usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo {Regional Oversight Mechanism of the Peace, Security and Cooperation framework for the Democratic Republic of Congo and the Region}.

 

 Mheshimiwa Waziri Mwijage (Mb.) alimwakilisha Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Ngazi ya Wakuu wa nchi wakati  Mheshimiwa Dkt Ndumbaro (Mb.) alimwakilisha Mhe. Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri.