Resources » News and Events

Rais Dkt. Magufuli afanya mazungumzo na Rais Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam

Mhe. Yoweri Museveni Rais wa Uganda akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Serikali waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam Rais Museveni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mashariki amefanya ziara ya siku moja ya kikazi nchini. Rais Museveni akizungumza na wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Dkt. Magufuli, alieleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kumpa taarifa Rais Magufuli kuhusu masuala yanayojiri kwenye mkutano wa BRICS uliofanyika Afrika Kusini. Katika mkutano huo ambao Afrika Mashariki ilishiriki kama kanda, Rais Museveni alitumia nafasi hiyo kuzishawishi nchi wanachama wa BRICS kuja kuwekeza Afrika Mashariki katika sekta za miundombinu ya uchukuzi na viwanda. Aidha, Rais Museveni amempongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kufufua Shirika la ndege la Tanzani ambalo litaleta mchango mkubwa katika kukuza utalii nchini.

Rais Dkt. Magufuli afanya mazungumzo na Rais Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam

  • Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifurahi pamoja na wananchi waliojitokeza kumuaga Rais Museveni wa Uganda uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam
  • Mhe. Yoweri Museveni Rais wa Uganda akizumgumza na wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam
  • Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya mazungumzo na Mhe. Yoweri Museveni Rais wa Jamhuri ya Uganda yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  • Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akijadili jambo na Mhe. Amelia Kyambade Waziri wa Biashara, Viwanda, na Ushirika wa Uganda
  • Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia mkutano uliokuwa ukiendelea