Prof. Kabudi azungumza na Uongozi wa Airtel jijini Dodoma.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) leo tarehe 10 Aprili,2019 Jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi Airtel ukiongozwa na Bw. Mukesh Bhavnani, Mwanasheria wa Bharti Airtel, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Bw. Sunil Colaso na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi. Beatrice Singano.

Katika mazungumzo hayo, Uongozi wa Airtel umemuhakikishia Mheshimiwa Kabudi kuwa Kampuni ya Bharti Airtel itaendelea kuwa Mbia mzuri na Serikali na kwamba wataendelea kupanua wigo wa huduma zao katika maeneo yote nchini na kuhakikisha hudua hizo zinakuwa za viwango na nafuu kwa watumiaji. Na kwamba mpango wao wa uwekezaji na kupanua wigo wa huduma zao hususan maeneo ya vijijini utakuwa moja ya chachu ya maendeleo ya kiuchumi nchini.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Kabudi pamoja na kuwashukuru kwa kumtembelea ameihakikishia Bharti Airtel kuwa Serikali iko tayari kuendelea na ubia walionao na iko tayari kuendelea kushauriana na kushirikiana namna bora ya kuimarisha ubia huo ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa na viwango na zinafika katika maeneo mengi nchini kwa gharama nafuu.
 

  • Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi,Zanzibar pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wakifuatilia Mkutano wa 9 wa Jumuiya hiyo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Dar es Salaam,Tanzania. Kutoka kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa akifuatiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Aman Abeid Karume,akifuatiwa na Makamu wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu Dkt Mohamed Gharib Bilali,akifuatiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo.