Prince William wa Uiingereza awasili nchini

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt Hamis Kigwangala(Mb.), akisalimiana na Mjukuu wa Malkia "Prince" William wa Uingereza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kiamataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ziara ya siku nne.  “Prince” William akiwa nchini pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Aidha, atatembelea kikosi cha Maji cha Jeshi la Polisi; Bandari ya Dar es Salaam; Jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House); Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga na Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro.

  • PrincePrince" William akisalimiana na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb.) mara baada ya kuwasili nchini.
  • Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Bw. Jestas Nyamanga naye akisalimia naKaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga naye akisalimia na "Prince" William.