Resources » News and Events

Naibu Waziri wa Kilimo wa China atembelea Tanzania

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt.Charles Tizeba ( Katikati mwenye kipaza sauti), akiongoza mazungumzo wakati wa Mkutano na Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Mhe. DK QU DONGYU(hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) tarehe 25 Januari,2018. Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania China Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki ( wa kwanza kulia), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt.Thomas Kashilila, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (wa pili kutoka mwisho kushoto). Katika majadiliano hayo pande zote mbili zimekubaliana kuundwa kikosi kazi ambacho kitakuwa na kazi ya kuhakikisha maeneo waliyokubaliana kushirikiana yanatekelezwa, kikosi kazi hicho kitahusisha wataalam kutoka Tanzania na China. Baadhi ya maeneo ambayo China na Tanzania watashirikiana ili kuinua kilimo cha Tanzania ni; kuboresha miundombinu ya Kilimo kama vile Scheme za Umwagiliaji, ushirikiano kati ya chuo cha Kilimo cha Sokoine na vyuo vya kilimo vya China, kushirikiana katika tafiti mbalimbali, China kuwekeza katika viwanda vya kuongeza thamani katika mazao, masoko n.k. Mhe. DONGYU anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 28, Januari,2018.

Naibu Waziri wa Kilimo wa China atembelea Tanzania