Naibu Mawaziri watembelea Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Mtukula.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Julius Wandera Maganda katika Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja mpakani cha Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda Tarehe 7 Februari 2019. Mara baada ya kukutana walipata fursa ya kutembelea na kujionea namna kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani cha Mtukula (OSBP) kinavyofanya kazi na kufanya Mkutano wa pamoja uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka Tanzania na Uganda. Mkutano huo umefanyia Mpakani mwa Tanzania na Uganda eneo la Mtukula

  • Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Waganda kabla ya kufanya mkutano wa pamoja na wadau mbalimbali. Wengine katika picha ni wajumbe walioongozana na Naibu Mawaziri hao.Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Waganda kabla ya kufanya mkutano wa pamoja na wadau mbalimbali. Wengine katika picha ni wajumbe walioongozana na Naibu Mawaziri hao.
  • Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakimsikiliza Afisa wa ukusanyaji mapato kutoka Tanzania Bw. Mohamed Shamte alipokuwa akielezea namna kituo hicho cha pamoja kinavyo fanya kazi. Naibu Mawaziri hao walijione namna watendaji wanavyofanya kazi kwa umakinDkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakimsikiliza Afisa wa ukusanyaji mapato kutoka Tanzania Bw. Mohamed Shamte alipokuwa akielezea namna kituo hicho cha pamoja kinavyo fanya kazi. Naibu Mawaziri hao walijione namna watendaji wanavyofanya kazi kwa umakin