Naibu Balozi wa Israel nchini Mhe. David Eyal atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye  makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David alipotembelea Taasisi hiyo jana  (5/11/2018) kwa ajili ya  kuona kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child Heart - SACH) la nchini Israel kwa kushirikiana na JKCI. Jumla ya watoto 85 wanatarajiwa kufanyiwa uchunguzi, upasuaji wa moyo wa kufungua na bila kufungua kifua.