Mkutano wa Pamoja kati ya Wizara na Ubalozi wa China nchini wafanyika

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda akifungua Mkutano wa Pamoja kati ya Wizara na Ubalozi wa China hapa nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, tarehe 8 Februari,2018. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango - Zanzibar, Bw. Khamis Mussa Omar, wengine ni watendaji na Maafisa kutoka taasisi mbalimbali za Serikali. Lengo la Mkutano huu pamoja na mambo mengine ni kukubaliana njia ya kufuatilia utekelezaji wa masuala mbalimbali katika maeneo ya Ushirikiano kati ya nchi hizi mbili. Akiongea katika Mkutano huu Prof. Mkenda amesema juhudi hizi zitasaidia kufuatilia na kugundua changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali kati ya Tanzania na China na kuzitatua kwa pamoja ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ambayo Tanzania na China tumekubaliana katika maeneo mbalimbali, ili wananchi wa nchi hizi mbili kunufaika na Ushirikiano huu wa kihistoria. Mkutano huo ulihudhuriwa na Viongozi na Maafisa kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali Serikali.

Mkutano wa Pamoja kati ya Wizara na Ubalozi wa China nchini wafanyika 

  • Balozi wa China nchini Mheshimiwa Wang Ke, ( katikati) akiongea katika Mkutano huo, wengine ni Maafisa kutoka Ubalozi wa China nchini alioambatana nao.
  • Katibu Mkuu Prof. Adolf Mkenda ( wa kwanza kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Ustralasia Bibi Justa Nyange, Bw. Joseph Kiraiya kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Mkrugenzi Mkuu wa EPZA Kanali Mstaafu Joseph Simbakaria na wengine ni Maafisa kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali wakifuatilia Mkutano huo