Resources » News and Events

Mkutano wa 8 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi wafikia tamati

Mkutano wa 8 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki wafikia tamati jijini Arusha

Mkutano huu uliofanyika kuanzia Aprili 28 hadi Mei 5, 2018, kabla ya kuhitimishwa ulitanguliwa na mikutano ngazi ya Wataalamu, ngazi ya Makatibu Wakuu na hatimaye Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta.

Pamoja na mambo mengine lengo la Mkutano huu lilikuwa ni kufanya mambo yafuatayo:-

kupokea na kujadili taarifa ya hali ya utekelezaji wa maamuzi yaliyofanywa na Mkutano uliopita wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi;
Kupokea na kupitia taarifa ya Kamati ya Takwimu;
Kupokea na kujadili taarifa ya Kikosi kazi cha kuandaa muswada wa kuanzishwa kwa taasisi za Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;
Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Masuala ya Fedha; na
Kujadili taarifa ya mapendekezo ya utekelezaji wa Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha, Mkutano huu umefanikiwa kupata ufumbuzi wa masuala kadhaa ya kichumi na fedha ambayo yanalenga kuboresha na kurahisisha mazingira ya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Downloads File: