Resources » News and Events

Meli ya Mfame wa Oman yawasili Jijini Dar es Salam kwa ziara

Meli ya Mfalme wa Oman " Fulk Al Salaam" imewasili leo Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya siku sita inayotarajiwa kumalizika tarehe 21 Oktoba, 2017. Meli hiyo imewasili na Mjumbe Maalum wa Mfalme, Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Mhe. Dkt. Hamad Al Rumphy Mahammed ambaye ameambatana na watu zaidi ya mia tatu (300) kutoka katika sekta mbalimbali.

Meli ya Mfame wa Oman yawasili Jijini Dar es Salam kwa ziara

  • Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akisalimiana na Waziri Mahammed katika sherehe za mapokezi zilizofanyika Bandarini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage.
  • Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Dkt. Aziz Mlima akisalimiana na Mhe. Dkt. Mahammed.
  • Viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Tanzania na Oman wakijadiliana ndani ya Meli.