Mazungumzo ya pamoja baina ya Mhe. Dkt Mahiga na Balozi Zhui mwakilishi wa FOCAC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amekutana na Balozi Zhui Yuxiao, Mwakilishi kutoka China anayesimamia masuala ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Wawili hao walijadili utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa FOCAC uliofanyika Beijing mwezi Agosti 2018.  Wamekubaliana kuundwa kwa kamati ya utekelezaji ambayo itaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ambapo Wizara imetakiwa pia kuteua mtumishi mmoja mwandamizi awe mratibu wa masuala ya FOCAC.