Resources » News and Events

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan afanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Viwanda (UNIDO), Mh. Li Yong, ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku tatu. Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb.)na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb.). Mazungumzo hayo yamefanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, tarehe 08 Machi,2018.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan afanya mazungumzo na  Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO.

  • Mhe. Samia Suluhu akimsikiliza Mhe. Yong wakati wa mazungumzo hayo
  • Mazungumzo yakiendelea kati ya Mhe. Suluhu na Mhe. Yong, wa kwanza kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mwijage akifuatilia mazungumzo hayo.