Resources » News and Events

Katibu Mkuu afanya ziara katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Namanga

Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (wapili kulia) akiwa na Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya (wapili kushoto) katika ziara ya kutemebelea OSBP Namanga Pro. Mkenda katika ziara hiyo aliambatana na Dkt.Susan Koech Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Maendeleo ya Ushoroba wa Kati kutoka nchini Kenya. Wawili hao kwa pamoja sambamba na kutembelea maeneo mbalimbali ya kituo hicho katika pande zote mbili za Tanzania na Kenya walipata fursa ya kuongea na watendaji wanaohudumu katika kituo hicho. Lengo la ziara hii ilikuwa nikuangalia ufanisi wa kituo hicho katika kusaidia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na watu kutika pande zote mbili za Tanzania na Kenya hivyo kurahisisha shughuli za biashara. Vilevile ziara hii ililenga kubaini changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho na kupelekea kushindwa kutoa huduma kwa ufanisi kwa wananchi wanaotumia kituo hicho. Aidha Makatibu Wakuu hao wamezipongeza Mamlaka na Taasisi zote zilizopo katika kituo hicho kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhudumia wananchi.

Katibu Mkuu afanya ziara katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Namanga

  • Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (watatu kushoto), akisikiliza maelekezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wanaohudumu katika Kituo hicho
  • Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akiwa nana Katibu Katawala wa Halmashauri ya Longido Bw.Toba Nguvila (kushoto) na Mwenyeketi wa Wafanyabiasha Namanga (katikati) wakiwa katika ziara za kutembelea kituo cha OSBD