Resources » News and Events

Katibu Mkuu afanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Nguyen Doanh, tarehe 09 Mei,2018, Jijini Dar es Salaam. Balozi Doanh alitumia fursa hii kujitambulisha na kumpongeza Prof. Mkenda kwa kuteuliwa kuwa Katibu mkuu wa Wizara. Aidha, mazungumzo hayo pia yalilenga kuboresha mahusiano yaliyokuwepo kati ya Tanzania na Vietnam, pia Prof.Mkenda amemhakikishia Balozi ushirikiano kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini.

Katibu Mkuu afanya mazungumzo na Balozi wa Vietnam nchini

  • Balozi Doanh naye akifafanua jambo katika mazungumzo hayo.