Katibu Mkuu afanya mazungumzo na Balozi wa Ujerumani nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda(kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Detlef Waechter alipomtembelea wizarani tarehe 9 Mei,2018, Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine mazungumzo hayo yalilenga katika kuendelea kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na Ujerumani.

Katibu Mkuu afanya mazungumzo na Balozi wa Ujerumani nchini

  • Mazungumzo yakiendelea, wanaofuatilia mazungumzo hayo ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy( Katikati kulia), kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Justus Nyamanga na kulia kwake ni Afisa Mambo ya Nje, Bi Lilian Kimaro.