Dkt. Ndumbaro Apokea Nakala za Hati za Utambulisho

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Brazil, Mhe. Antonia Augusto Cesar leo jijini Dar Es Salaam. Baada ya kupokea hati hizo, Dkt. Ndumbaro alifanya mazungumzo na Balozi Mteule, Mhe. Cesar ambapo aliahidi kuwa Serikali itampa ushirikiano ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, alimweleza vipaumbele vya Serikali ya awamu tano na kuiomba Brazil iunge mkono katika kufanikisha vipaumbele hivyo.