Dkt. Ndumbaro afanya mazungumzo na balozi wa Italia nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Damas Daniel Ndumbaro(Mb.), amefanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Mheshimiwa Roberto Mengoni katika ofisi za wizara Dodoma. Katika mazungumzo hayo, miongoni mwa mambo mengine, Tanzania na  Italia zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika sekta za uwekezaji, utalii pamoja na  kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia.  

  • Katibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Charles Faini (wa kwanza na kulia) na Afisa wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Kisa Mwaseba (wa mwisho kushoto),Katibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Charles Faini (wa kwanza na kulia) na Afisa wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Kisa Mwaseba (wa mwisho kushoto),