Dkt. Ndumbaro aapa kuwa Mbunge wa EALA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro(Mb) ameapishwa rasmi kuwa Mbunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika tukio hilo Dkt. Ndumbaro alisindikizwa na Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe na Mhe Pamela Maasay kutoka Tanzania. Aidha, mara baada ya kuapishwa alishiriki kikao cha Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (East Africa Legislative Assembly - EALA), ambalo lilijadili na kupitisha muswada wa Sheria ya kuanzisha Taasisi ya Takwimu ya Afrika Mashariki, tukio hilo limefanyika kwenye Bunge la Afrika Mashariki jijini Arusha.

  • Dkt. Ndumbaro akiwa tayari kwa vikao vya Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kuapishwa.