Dkt. Mahiga akutana na Viongozi kutoka Norway, Denmark, Venezuela na China

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga wa pili kutoka kushoto ukiwa katika mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam leo. Viongozi hao walijadili namna ya kukuza na kuimarisha ushirikiano hususan wa kibiashara ikiwemo mchakato wa kampuni ya Equinor wa kuzalisha gesi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kusafirisha nje ya nchi

  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiagana na mgeni wake, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe. Nikolai Astrup baada ya kufanya mazunguzmo ambayo yalikuwa ya mafanikio makubwa katika mustakabali wa Tanzania na Norway.