Balozi wa Palestina amekutana na Dkt. Ndumbaro

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hamdi Abduli, katika mazungumzo yao yaliyojikita kwenye kukuza zao na soko la Korosho nchini Tanzania, ambapo Palestina wanauhitaji wa bidhaa ya korosho. 

Pia Mhe. Hamdi Abduli amemshukuru Dkt. Ndumbaro kuwa ushirikiano anaoupata kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  wakati wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini

  • Balozi wa Abduli pamoja na Dkt. Ndumbaro wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Mambo ya Nje.