Balozi Mahiga;Tanzania itaendelea kushiriki katika ulinzi wa amani duniani

Wakitoa heshima kwa ajili ya kuwakumbuka Walinda Amani, waliosimama mbele kutoka kushoto ni Mhe. Waziri Mahiga akiwa na Mwakilishi kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Maj. Gen. Henry Kamunde, Bw. Alvaro Rodriguez na Mwakilishi kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, Kamishna Nsato Marijani. Siku ya Walinda Amani Duniani huadhimishwa tarehe 29 Mei ya kila mwaka ambapo kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa: Miaka 70 ya huduma na kujitoa (UN Peacekeeping: 70 Years of Service and Sacrifice). Katika hotuba yake, Mhe. Waziri Mahiga alieleza kuwa yapata miaka 12 tangu Tanzania ianze kushiriki katika ulinzi wa amani chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. Pia akasisitiza Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inasaidia kupatikana kwa amani katika mataifa mengine kwakuwa hakuna taifa linaloweza kufanikiwa katika maendeleo pasipo kuwepo na amani ya uhakika. " Sio jambo rahisi kukubali kutoa uhai wako kwa ajili ya mtu mwingine lakini Tanzania itaendelea kuungana na mataifa mengine duniani katika kusaidia kupatikana kwa amani ya mataifa hayo" alisema Mhe. Mahiga. Aidha, Katika kuwakumbuka Walinda Amani wote Duniani waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao, pamoja na kutoa heshima kwa wale ambao bado wanaendelea na jukumu la kulinda amani, Tanzania imepoteza jumla ya askari wapatao 30 ndani ya miaka 10, pia dunia imepoteza zaidi ya askari 3500 na kwa sasa Tanzania inajivunia kuwa na jumla ya askari wapatao 2,600 wanaohudumu katika misheni sita (6) za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa.

Balozi Mahiga;Tanzania itaendelea kushiriki katika ulinzi wa amani duniani

  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika maadhimisho ya miaka 70 ya Siku ya Walinda Amani Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa vya Mnanzi Mmoja Jijini Dar es Salaam tarehe 29 Mei 2018.
  • Mhe. Waziri Mahiga akiweka shada la maua katika Mnara wa Mashujaa uliopo Viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wa Walinda Amani Duniani.