Home » The Press » Waziri Mkuu wa India kutembelea Tanzania
RSS News
Waziri Mkuu wa India kutembelea Tanzania
Posted: Wednesday May 25, 2011 3:59 PM BT
Waziri Mkuu wa India, Mhe. Dkt. Manmohan Singh anatarajia kuwasili nchini tarehe 26 Mei, 2011 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Ziara hiyo ya Mhe. Dkt. Singh inafuatia mwaliko wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Mkuu wa India, Mhe. Dkt. Manmohan Singh anatarajia kuwasili nchini tarehe 26 Mei, 2011 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Ziara hiyo ya Mhe. Dkt. Singh inafuatia mwaliko wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Dkt. Singh ambaye atawasili siku hiyo saa 10.00 jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, atapokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Akiwa hapa nchini, Mhe. Dkt. Singh anatarajia kukutana kwa mazungumzo rasmi na Mhe. Rais Kikwete tarehe 27 Mei 2011, ikifuatiwa na kusainiwa kwa mikataba mbalimbali ya ushirikiano baina ya Tanzania na India. Aidha, siku hiyo ya tarehe 27 Mei 2011, Mhe. Dkt. Singh kwa pamoja na Mhe. Rais Kikwete watakutana na Waandishi wa Habari kabla ya kushiriki dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa heshima yake na Mhe. Rais Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.

Mhe. Dkt. Singh pia anatarajia kutembelea Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) kwa ajili ya kuzindua mradi wa Kituo cha Ubora katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (India-Tanzania Centre of Excellence in Information and Communication Technology) ulioanzishwa chuoni hapo kwa ushirikiano wa nchi hizi mbili.

Mhe. Dkt. Singh anatarajia kuondoka hapa nchini tarehe 28 Mei, 2011 kurejea nchini kwake India.