Home » Highlights » Mkutano wa Mawaziri wa Nje wa Nchi za Afrika na Uturuki
RSS News
Mkutano wa Mawaziri wa Nje wa Nchi za Afrika na Uturuki
Posted: Friday December 16, 2011 11:34 PM BT
image

Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (pichani), akisoma tamko la Tanzania katika mkutano wa siku mbili wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Uturuki unaofanyika mjini Instabul, nchini Uturuki.

Madhumuni ya Mkutano huu ni kupitia mkutano wa kwanza wa mwaka 2008 uliohudhuriwa na Wakuu wa Nchi za Afrika na Uturuki, na kutathmini maendeleo ya ushirikiano baina ya nchi hizo (Africa - Turkey Partnership).

Awali, Wakuu wa Nchi wa pande zote mbili waliridhia mpango wa ushirikiano na kuainisha maeneo tisa (9) ya miradi mbalimbali ambayo ni muhimu katika ushirikiano huo. Maeneo hayo ni pamoja na miradi ya biashara na uwekezaji, ushirikiano wa kidiplomasia, mazingira, miradi ya afya na miundombinu, na miradi mingine.

Tafadhali bofya hapa chini kusoma tamko hilo la Mhe. Waziri Membe:

MFAICs_Statement_in_Istanbul_2011.doc